TIMBULO ASIMULIA MKASA MZIMA WA KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA
Tangu jana kumekua na story zilizoenea mitaani kuhusu Mwanamuziki Timbulo
kukamatwa na madawa ya kulevya Nchini Burundi. Picha zake zilizagaa katika mtandao wa facebook zikimuonyesha timbulo
akiwa chini ya ulinzi wa police na kidhibiti chake cha madawa haya
ambayo yamefungwa kwa mfano wa pipi...
Ilinibidi nimtafute timbulo
kupitia mtandao wa whatsup ambapo nilimuona akiwa active kama dkk kumi
zilizopita mara baada ya kupata habari hizo
Timbulo amesema ni
kweli alihisiwa kuwa amebeba madawa ya kulevya kitu kilichowafanya
wanausalama kuomba kumkagua na kweli kumkuta na Pipi ambazo mara nyingi
zimekua ni mfumo wa kubebea madawa ya kulevya katika begi lake, lakini
katika maelezo ya timbulo anasema hazikuwa dawa za kulevya kweli bali ni
mfano wa dawa ambazo alifanyia shooting katika movie yake ya hivi
karibuni na kusahau kuzitoa.
Hata hivo kutokana na maelezo yake anasema
alihisiwa zaidi kubeba mzigo huo kutokana na mtu aliekuja kumpokea
kusadikika kuwa katika biashara hiyo.
Timbulo alikua nchini
burundi kwa shughuli zake za kimuziki akiwa ametokea Bukoba alikokua na
shows huko lakini pia ikiwa ni mwendelezo wa safari ya kumfikisha Younde
Cammeron ambako pia alikua anaenda kwa shughuli zake za kimuziki. Safari
zote hizo ziliishia hapo baada ya tukuo hilo na hivi mpaka naingia
mtamboni timbulo aliniambia yupo jijini mwanza kwa safari ya kurudi Dar
Es Salaam
No comments:
Post a Comment