
Naiona hatari kubwa nyingine inakuja mbele yetu. Ni haya makundi mawili; MaBodaboda na MaMachinga.
Hofu yangu kuna
wanasiasa wachache wanaowaona vijana hawa, katika matatizo yao ya
kiuchumi, kuwa ni mtaji wa kisiasa. Na kimsingi wanawageuza kuwa ‘ Shuka
za Kisiasa’. Na hapa ni wanasiasa wa vyama vyote.
Hatari yake?
Viongozi wasipokuwa makini, wakaacha kutanguliza busara na hekima kwenye kauli zao, basi, hofu ya kauli kupelekea machafuko na kuvunjika kwa amani itabaki kuwepo.
Viongozi wasipokuwa makini, wakaacha kutanguliza busara na hekima kwenye kauli zao, basi, hofu ya kauli kupelekea machafuko na kuvunjika kwa amani itabaki kuwepo.
Maana, hawa
MaBodadoba na MaMachinga, pamoja na kuwa wengi wao ni vijana wema
kabisa, na ambao, kwenye mahangaiko yao, kama wagonjwa, wanamsikiliza
kila anayekuja na kauli za kuwapa matumaini, hata kama ni ya muda
mfupi, na hata kama ni kwa kuvunja sheria.
Na kwa vile Elimu ya
Uraia iko chini sana katika jamii yetu, hata kwa miongoni mwa viongozi
wetu, basi, ndio maana naiona hatari hii kubwa inayokuja mbele yetu.
Kwamba MaBodaboda na MaMachinga wakiendelea kutumiwa kama ‘ Shuka za
Wanasiasa’, basi, yumkini, huko tuendako Watanzania tujiandae na kazi ya
kuchimbiana makaburi. Maana, siku zote, maovu huzaa maovu.
MBodaboda au Mmachinga mmoja akiuawa, kuna mia watakaokuja kutaka
kulipiza kisasi. Na Polisi mmoja akiuawa, kuna operesheni ya kipolisi
itakayofuata.
Na polisi wetu hawa ni vijana hawa hawa ambao wengine
wameponea chupuchupu kuwamo kwenye makundi haya ya MaBodaboda na
MaMachinga, lakini sasa, tumewapa pia silaha za moto wabebe.
Naam, tukichoka kuhubiri Amani, Upendo Na Mshikamano, basi, tujiandae na kazi ya kuchimbiana makaburi.
No comments:
Post a Comment