HUKUMU YA KAJALA YAPIGWA KALENDA



Hukumu iliyokuwa ikisubiliwa na baadhi ya wadau wa tasnia ya sanaa hususani upande wa filamu ya msanii wa bongo movi Kajala Masanja imehairishwa mpaka tarehe 25 mwezi wa tatu

Chanzo cha habari ambacho ni mmoja wa rafiki wake wa karibu na msanii huyo alieleza kuwa kutokana na kutokuwepo kwa baadhi ya wahusika katika kesi hiyo imemladhimu hakimu kuihairisha kesi hiyo mpaka tarehe iliyopangwa hapo juu.







...............................................................................................................
 
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam juzi (Jumatano) kupitia wakili wa serikali, Leonard Swai ilisema inatarajia kuwafikisha mashahidi 13 mahakamani hapo kutoa ushahidi katika kesi inayomkabili staa wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja na mumewe Faraja Chambo.
Katika kesi hiyo ya kuuza nyumba iliyopatikana kwa njia ya rushwa na kuwekewa kizuizi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ambayo ipo katika hatua za awali, Wakili Swai aliwauliza washitakiwa maswali kadhaa ikiwemo kama kweli ni wanandoa ambapo walikiri kuwa mke na mume.
Swali lingine waliloulizwa washitakiwa hao ni kama kweli walimuuzia nyumba Emmilian Rugalila ambapo walikiri kufanya hivyo.
Washitakiwa hao walipoulizwa kama walifahamu kuwa nyumba hiyo iliwekewa kizuizi na Takukuru, walisema si kweli.
Baada ya maswali hayo, hakimu aliyekuwa akisiliza kesi hiyo, Sundi Fimbo alimuuliza mwendesha mashitaka huyo kama ana mashahidi wa kuthibitisha mashitaka hayo ambapo alijibu kuwa wapo mashahidi 13 walio tayari kufika mahakamani kutoa ushahidi wao.
Kufuatia kauli hiyo, Hakimu Fimbo aliahirisha kesi hiyo hadi Aprili 30, mwaka huu akimtaka mwendesha mashitaka huyo kuwapeleka mashahidi hao mahakamani hapo