Sports


LIVE MATCH CENTRE: YANGA SC 2 - 0 AZAM FC - YANGA MABINGWA WA KAGAME CUP


 90+2: Said Bahanuzi anafunga bao la pili na refa anamaliza mpia hapa. Yanga wanafanikiwa kuutetea ubingwa wao wa Kagame Cup.

87: Said Bahanunzi ananyeshwa kadi ya njano dakika ya 87
85: Dakika tano zimebakia mpira kumalizka, na Azam hawaonyeshi dalili yoyote ya ziada kutafuta bao la kusawazisha huku ukuta wa Yanga ukisimama imara vilivyo.

78: Azam wanamiliki zaidi mpira huku Yanga wakiwa wamerudi nyuma kupaki basi. George Blackberry Odhiambo anapiga shuti kali linalotoka nje sentimita kidogo kutoka langoni.

75: Yanga wanafanya mabadiliko anatoka Gumbo anaingia Juma Seif Kijiko. Mpira unaonekana kupooza na timu zote zikionekana kuchoka.

67: Azam wanafanya mabadiliko, anaingia Mrisho Ngassa anatoka Kipre Tchetche.

56: Yanga nao wanafanikiwa kufika ndani ya sita ya Azam nao wanafuata mkondo wa Azam na wanapoteza. Kwa kifupi timu zote zinatengeneza nafasi ya kufunga lakini safu zao za ushambuliaji zinakosa umakini na wanshindwa kuzitumia.

55: Azam wanaendelea kupoteza nafasi za wazi kuweza kufunga mabao.

DK 46: Kipindi cha pili kinaanza hapa.

45: Mpira ni mapumziko. Azam watajuitia nafasi walizopoteza, Yanga wanacheza wakiwa wanaonyesha hali ya kuutaka ushindi kwa hali na mali, tofauti na Azam wanaocheza wakiwa wame-relax kama tayari wameshinda.

DK 44: Azam wanafanya makosa ya kizembe hapa na Ibrahimu Shikanda anarudisha mpira mfupi nyuma unaomfikia Hamis Kiiza na anweka kimiani goli la kuongoza la Yanga.

DK 40: Rashid Gumbo analeta uhai sana kwenye safu ya mashambulizi ya Yanga - Azam wanacheza mpira zaidi katikati ya uwanja na wanalisogelea sana lango la Yanga lakini wanakosa umakini.

DK 35: Yanga wanalishambulia lango la Yanga na wanajaribu kwa kila kila hali kuweza kupata bao. Azam wenyewe wanacheza zaidi pasi huku wakipoteza nafasi nzuri za kufunga.

DK 30: Azam wanalisogelea sana lango la Yanga lakini wanashindwa kuzitumia nafasi wanazopata - Yanga wanaonekana tishio sana wanapofika kwenye lango la Azam na lolote linaweza kutokea hapa.

DK 20: Timu zote zinashambuliana kwa zamu, japo Azam wanaendelea kutawala sana safu ya kiungo. Yanga 0 - 0 Azam.

DK 15: Yanga 0 - 0 Azam

DK 10: Azam wanaonekana kumiliki mpira zaidi katika dakika hizi 10 za mwanzo, huku Yanga wakicheza vizuri nyuma na wakishambulia kwa counter attack.

DK 02: Azam wanalishambulia lango la Yanga na John Bocco anakosa goli baada shuti alilopiga kupaa juu ya lango.


DK 01: Mechi ndio inaanza hapa - Azam 0 - 0

Timu ndio zinaingia uwanjani na zinajipanga kukaguliwa. Yanga kama kawaida wamevaa jezi za njano na Azam wamevaa nyeupe.

1.Ally Mustapha 'Barthez' - 1
2.Stephano Mwasika - 3
3.Oscar Joshua - 4
4.Nadir Haroub 'Cannavaro' (C) - 23
5.Kelvin Yondan - 5
6.Athuman Idd 'Chuji' - 24
7.Rashid Gumbo - 16
8.Haruna Niyonzima - 8
9.Said Bahanunzi - 11
10.Hamis Kiiza 'Diego' - 20
11.David Luhende - 29

Subs:
1.Yaw Berko - 19
2.Ladislaus Mbogo - 28
3.Juma Seif 'Kijiko' - 13
4.Idrisa Rashid - 12
5.Shamte Ally - 15
6.Nizar Khalfan - 7
7.Jeryson Tegete - 10

Head Coach: Tom Saintfiet
Ass Coach : Fred Felix Minziro
Goalkeeper Coach: Mfaume Athuman
Team Doctor : Dr Suphian Juma
Kit Manager : Mahmoud Omary (Mpogolo)
Massagist : Jacob Onyango
Team Manager : Hafidh Saleh