HUYU NDO BINTI ALIYETOROKEA UINGEREZA AKIKWEPA KUTOMASWA NA MFALME MSWATI
Msichana
mdogo ameomba hifadhi ya ukimbizi nchini Uingereza baada ya kukataa kwa
dharau harakati za ndoa za wake wengi za Mfalme Mswati III wa Swaziland
na kugoma kujiunga kwenye nyumba harimu ya wake 13.
Tintswalo Ngobeni, mwenye umri wa miaka 22, alitimkia Uingereza kutoka taifa hilo la kusini mwa Afrika akiwa na umri wa chini ya miaka 18 baada ya kuvuta hisia za mfalme huyo milionea, mtawala maarufu mkandamizaji kwa maisha yake ya anasa.
Ikiwa ni sehemu ya mila za Swazi, Mfalme Mswati III, mwenye umri wa miaka 45, anaruhusiwa kuchagua mke mpya kila mwaka.
Tintswalo, ambaye sasa anaishi mjini Birmingham, alikuwa na umri wa miaka 15 tu wakati Mfalme huyo alipofanya harakati zake baada kumuona kwenye jumba la kifalme la mke wake wa nne, LaNgangaza. Binti huyo alisema 'alitishika' pale alipogundua dhamira zake za ndoa.
Tintswalo alikuwa amelazimishwa kuachana na maisha ya starehe kwenye shule moja ya bweni huku shangazi yake, ambaye alikuwa mlezi wake mkuu, akisuka mipango ya kutorokea Uingereza kuungana na mama yake, ambaye alihamia mjini Birmingham miaka mitano kabla, akimtoroka mume wake mnyanyasaji.
"Sikuwa na jinsi," alisema. "Hakuna aliyewahi kumwangusha mfalme huyo au kuthubutu kumdharau, hivyo nikatoweka tu."
Tangu kuwasili nchini Uingereza, Tintswalo amekuwa sauti ya upinzani dhidi ya utawala kandamizi za Swazi, ambapo vyama vya upinzani vya siasa vimefungiwa na wanaharakati wamekuwa wakikamatwa mara kwa mara au kushambuliwa.
Hatahivyo, shughuli kuu za Tintswalo, ikiwamo maandamano ya kila wiki nje ya ubalozi wa Swazi mjini London akiwa na kikundi cha Swazi Vigil, zimesikika kwa mamlaka hizo nchini kwake na sasa anaamini yuko kwenye hatari kubwa zaidi kuliko ilivyowahi kutokea.
Alisema: "Hivi karibuni nilipata taarifa kwamba watu wametumwa kutoka Swaziland kuja kunikamata, jambo ambalo hakika linanitisha mno. Kama nikirejea, nitakamatwa au mbaya zaidi huku pale kuna watu ambao wanateseka, kupigwa au kuuawa kwa kujihusisha na siasa."
Tintswalo sasa anaishi katika mashaka ya kuweza kurejea nchini Swaziland, baada ya ombi lake la kwanza la hifadhi ya kisiasa nchini Uingereza mwaka 2007 kukataliwa mwaka 2011.
Mwezi uliopita, alikamatwa na kupelekwa kwenye kituo cha kushikilia wahamiaji baada ya miezi 18 ya kuripoti kila wiki katika mamlaka hizo.
Hatahivyo, baada ya shinikizo kutoka TUC na ofisi ya Mbunge wa Birmingham kupitia chama cha Labour, Roger Godsiff, Tintswalo aliachiwa na sasa amekata rufaa wizara ya Mambo ya Ndani.
Godsiff alisema juzi: "Tumefurahishwa mno wanasheria walifanikiwa sana katika kuwezesha kutazamwa upya kwa kesi ya Ngobeni."
Baba huyo wa watoto 27, Mfalme Mswati III alikuwa mgeni kwenye harusi ya William na Kate na pia kwenye sherehe za Miaka 50 ya Malkia wakati wa majira ya joto mwaka jana.
Mke wa sita wa mfalme huyo alitoroka kutoka kwenye jumba hilo harimu mwaka jana, akielezea miaka kadhaa ya 'machungu na udhalilishaji wa kimwili' uliofanywa na mume wake.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani alikataa kuzungumzia chochote.
AIBU:HUU NDO UCHAFU ULIOFANYWA NA MSANII DIAMOND KATIKA SHOW YA FIESTA DAR.....WENGI WADAI KUWA YEYE NI SHOGA
Kwa wale walioondoka mapema kwenye show ya Fiesta usiku wa kuamkia Jumapili baada tu ya Rick Ross kumaliza performance yake, walikosa kujionea kituko kilichofanywa na Diamond Platnumz. Ama wengine wamekuja tu kuona picha zilizosambaa kwenye internet
Akiwa stage na madancer wake wakati show imepamba moto, Diamond aliamua kuvua na kuonesha boxer yake nyeupe kama ishara kuwa yeye na madansa wake ni ‘wasafi’ kiasi cha kutoogopa kuionesha hadharani.
Bahati mbaya watanzania wamemuelewa tofauti. Kitendo hicho kimewakera wengi.
Kwa mujibu wa maoni tuliyoyapata kupitia ukurasa wetu wa Facebook baada ya jana kuweka picha hiyo, wengi wameitafsiri picha hiyo kama ishara ya ‘ushoga’ na huku wengine wakienda mbali zaidi na kuibua tena mada ya ufreemason. Haya ni baadhi ya maoni.
“Wanaonyesha kuwa na mapepo hao maana walianza na kuvua magoti hadi
mashati wakabakiza suruali , sasa wamebakiza boxer unadhani wakishatoa
boxer watabakiza nini, huo ni ushirikina na muda si mrefu watahumbuka
hao maana naona ule mwisho wao umeshafika; hizo ni akili ama matope…wana
akili ama matahairaaaaa1.”
“Ndio maana wazee wetu hawaupend kuusikiliza huu muzk munaoita bongo
flava. Uchafu kama huu mnafanya mbele za watu au umaarufu unatafutwa kwa
kila njia,basi huyo tanzanite awe john elton wa bongo.”
“Lbd alielewa tofauti,alpockia MUONEKANO MPYA BURUDAN ILEILE ndani ya
fiesta!!nd mana akafanya hcho k2ko lkn pia mayb woz search and luking
fo huzband! nadhan co rdhk nyota uyu.teh teh teh shame upon hiz
unimpressive kboxa.”
“Huu ni upuuzi wa wasanii wetu. Yaani huyu ndiye anayeitwa staa
ambaye hana hata chembe ya adabu?? Na ninyi mnaangalia tu
mnamshangilia???”
“OH! Lord hav marcy on this young man.This is devilish coz there s no any gud motivation to build up our society.Kwanini wasanii wa africa wanapenda kuiga utamaduni wa wa zungu? ambao haujengi jamii ye2 bali ina teketeza.kama we ni muimbaji kuja na stail ya utamaduni wako dnt promote someones cultur,mbona wao hawapromot utamaduni wenu,b yoself dnt try b somebody else,the moment u try to imitate frm someone u ll mess up coz u ll never b that person.U were created as a unique person so b u.”
“Nampenda diamond lakn kwa mambo haya mmh…. hapana kwakweli, sa
kulikua na haja gani ya kupanda jukwaan na nguo ta2 c wangeziacha2 home
wakaingia na hivo vchup au ndo vilikua vpya!!”
“What are they doing???/ is Diamond Freemasons..coz what they are
doing is inhuman..i don’t know that what am thinking..if dancing is like
that then we don’t have to…are u feeling happy watching something like
this…damn Diamond.”
“Soko la entertainment tz linagonga mlango wa shetani…bado mtayaona ya laana zaidi ili wafanikiwe..ni huruma sana coz hao waliotangulia kuingiza soko lao la burudani mikononi mwa shetani wanajuta na 2nashuhudia wanavyoendeshwa na wengine wakituonya kwa bidii,ila wabongo ndo wanakimbilia huko..they’ll sell their soul for money and fame..watch out fo that!”
CHEGE APATA AJALI, AJERUHIWA
Msanii wa Kigoma All Stars Chege Chigunda usiku wa jana amepata ajali mbaya ya gari maeneo ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Taarifa za awali kuhusu ajali hiyo
zimesema kuwa usiku huo Chege alikuwa ametokea jijini Nairobi kwa
shughuli kadhaa za kimuziki.
Katika mahojiano ya dakika chache na
mtangazaji wa Clouds FM, Diva kwenye kipindi cha Ala za Roho, Chege
amesema usiku huo wa saa nne akiwa kwenye gari alikutana pikipiki
katika mtaa mmoja wa maeneo ya Temeke ambaye alimgonga na yeye kupata
ajali hiyo , Chege amepata majeraha kadhaa lakini anaendelea vizuri
licha ya gari lake kuharibika vibaya maeneo ya mbele.
Hivi ndivyo gari la Chege lilivyokuwa baada ya ajali
Haikuweza kufahamika mara moja hali ya mtu huyo aliyekuwa na
pikipiki,Kupitia mahojiano hayo mafupi Chege amewatoa hofu mashabiki
wake kuwa hali yake ni nzuri na yupo salama.Hivi ndivyo gari la Chege lilivyokuwa baada ya ajali
Staa wa bongo fleva Naseeb Abdul 'Diamond' amempa pole mwanamuziki mwenzie huyo wa Kigoma All Stars kwa kilichotokea na kuwataka wasanii wengine kumtia moyo Chege
"Nampa pole mwanangu Chege Chigunda kwa ajali mbaya ya gari aliyopata ,Tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa yote yaliyotokea" alisema Diamond.
Baada ya kuamua kutokaa kimya kutokana na shutuma zilizotolewa dhidi yake na mpenzi wake wa zamani WEMA SEPETU, Mwimbaji DIAMOND PLATNUMS ameamua kutoa kauli yake ya mwisho kuhusu Wema.
Diamond anakiri kwamba hakutaka kabisa kumzungumzia Wema kwenye vyombo vya habari baada ya kuachana kwa sababu hakutaka malumbano lakini imebidi iwe hivyo kwa sababu ya hasira aliyoipata kutokana na Wema kuzungumza uongo mwingi dhidi yake.
Exclusive na millardayo.com Diamond amekiri kwamba aliachana rasmi na Wema mwezi january mwaka huu na hiyo ni kutokana na kukerwa na tabia za Wema alizozikemea lakini mwisho wa siku hakufanikiwa, zikawa zinaendelea…. ambapo tabia hizo ni pamoja na Wema kuwalipa waandishi wa habari wa magazeti ili watoe stori zake, japo Diamond alikua anawalipa waandishi wasiandike chochote, yeye alikua anawalipa zaidi.
Diamond amesema “kuna vitu vya chinichini alikua ananifanyia vya kuniumiza kama kudanganyana lakini nilikua sivipeleki kwenye vyombo vya habari kwa sababu nilikua namuheshimu namfichia kwa sababu anasema hafanyi hivyo, lakini akawa anaendelea kuvifanya kama kunidanganya kwenye mapenzi japo kudanganyana kwenye mapenzi ni kitu cha kawaida hata wapenzi wangu wa zamani walikua wananidanganya na mimi nawadanganya pia, lakini alikua anapeleka kila kitu kwenye magazeti hata vitu vya watu wawili ndani ya nyumba anavipeleka, sasa nyumba inakua haina siri”
Ameamplfy zaidi kwamba “Wema alikua anapeleka stori kabisa yani kitu tumefanya watu wawili ndani unashangaa kukikuta kwenye gazeti, nikikutana na waandishi ambao ni rafiki zangu wananiambia ebwana wewe unajisumbua bure yeye mwenzako akija hapa ndio anataka aandikwe, mimi nilishawahi kumkuta hotelini uchi kabisa akiwa na mwanaume mwingine hotelini mwishoni mwa mwaka jana lakini sikuongea chochote kwenye vyombo vya habari, nikamchukua na kuondoka, niliamua kumtunzia siri yake na nikanyamaza kwa kuichukulia kama mwanaume, na hata nikawa nikifika kwenye media nilikua nampamba na kumtetea kwamba jamani Wema hayuko hivyo na ni mstaarabu”
“Baada ya kumkuta niliumia sana lakini nikajua ndio mambo ya mapenzi ikabidi nivumilie, na ndio maana mimi naandika nyimbo nzuri kwa sababu nakutana na vitu vingi sana kwenye mapenzi” – Diamond
Diamond amefunga mjadala wa yeye na Wema kwa kuthibitisha kwamba hana ugomvi na Wema wala hana tena hisia za kimapenzi kwa mshindi huyo wa Miss Tanzania 2006, hawezi kurudiana nae kwa sababu kwa sasa imetosha na anampenzi mwingine ambae hata Wema anamfahamu.
Ishu yote hii imetokana na show aliyoifanya Diamond pale Mlimani City weekend iliyopita ambapo Diamond alikataa kupokea pesa Wema Sepetu aliyokua anampa pale kwenye stage kwa sababu ya kukwepa Drama, Na Wema hakua mpenzi pekee wa zamani wa Diamond aliekuwepo kwenye show, kulikua na warembo wengine wawili wa zamani wa Diamond lakini hao wote alipokea pesa zao.
Uhusiano wa Diamond na Wema umedumu kwa mwaka mmoja ambapo walipanga kuoana huku tayari Diamond akiwa amemvisha pete ya uchumba mrembo huyo ambae pia ni mwigizaji wa movie Tanzania.
Diamond amethibitisha kwamba Show yake ya DIAMONDS ARE FOREVER siku tatu kabla ya kufanyika, tayari ilikua imeuza ticket zote elfu moja na hivyo ukumbi kujaa, huku kila ticket ikiwa ni shilingi elfu 50…… show yake imekua show ya kwanza ya msanii wa kibongo kulipisha watu elfu 50 na bado ikajaza mapak watu wakakosa ticket, kwa swala la kiingilio amezishinda mpaka show za Jay Z & 50 cent ambazo zilifanyika bongo na watu kulipa elfu 25 – 30.
AIBU JACK WA CHUZI.......
MWANADADA
anayefanya vizuri kunako gemu la filamu Bongo, Jacqueline Pentezel
‘Jack wa Chuz’ amejikuta katika wakati mgumu baada ya kupigwa picha za
utupu na kusambazwa kila kona ya jiji.
Picha hizo zinamuonesha Jack akiwa kama alivyozawaliwa katika mapozi tofauti, jambo ambalo linaonesha kuwa alipigwa picha hizo na mpenzi wake.
Kikizungumza na Mpekuziblog, chanzo makini ambacho ni rafiki wa karibu na msanii huyo, kilisema Jack amekuwa akilalamika kuhusu kupotelewa na kadi iliyokuwa na picha zake za siri hivyo inawezekana aliyechukua ndiyo amezisambaza picha zisizofaa kuonekana hadharani.
“Kwa pozi hili aliloweka Jack inawezekana alipigwa na mpenzi wake kwa lengo la kujifurahisha kama wapenzi, mapozi aliyokaa yanathibitisha hilo kabisaa,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kuzitia picha hizo kibindoni, mtandao huu ulimtafuta Jack ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Jamani hizo picha sielewi zimevujaje maana kuna kadi yangu ya simu ilipotea ikiwa nazo, nilipigwa na mpenzi wangu kwa nia njema tu, si unajua mambo ya mapenzi tena… sasa kama zimeshafika kwenu sijui niseme nini tena hapo.”