Jitendra Sakhpal akisindikizwa na polisi kuingia mahakamani.
Msichana mdogo ameungua vibaya baada ya rafiki yake wa kiume aliyevunja
naye uchumba kudaiwa kumtega walipokutana, kumlazimisha kunywa tindikali
na kumsukumia kwenye bahari.
Ripoti nchini India zinadai msichana huyo hapo kabla alikuwa mpenzi wa
Jitendra Sakhpal, miaka 21, ambaye alikuwa amemchumbia, lakini alikataa
kuolewa naye na kusitisha mahusiano hayo sababu familia yake
haikumridhia mwanaume huyo asiye na ajira.
Baba wa msichana
huyo aliripotiwa kuieleza polisi kwamba mvulana huyo alikuwa
akiwasumbua, na ndugu mmoja wa kike alidai kwamba Sakhpal alitishia
kumuua baba wa msichana huyo, kwa mujibu wa ripoti hizo.
Msichana huyo, ambaye hakutajwa jina, anaripotiwa kuwa mahututi kwenye Hospitali ya Thunga, mjini Mumbai.
Sakhpal amekamatwa na kushitakiwa kwa jaribio la mauaji.
Shambulio
hilo limetokea Jumamosi huko Gorai Beach katika kitongoji cha magharibi
mwa Mumbai. Wote ni wakazi wa Dahisar mjini Mumbai.
Msichana
huyo mwenye miaka 18, mwanafunzi wa HSC ambaye ametokea Borivali,
alikutana na Sakhpal wakati akiondoka chuoni Jumamosi, kwa mujibu wa
Polisi.
"Jumamosi, Sakhpal alikutana na msichana huyo nje ya
chuoni kwake huko Gorai na kumtaka amsindikize kwa matembezi kidogo.
Wawili hao walipanda boti na kwenda kijiji cha Gorai," inspekta wa ngazi
ya juu Deepak Bagawe alieleza.
Inspekta huyo alisema Sakhpal
alijaribu kumshawishi mpenzi wake huyo wa zamani kurejesha mahusiano
yao, lakini pale binti huyo alipokataa alidaiwa kutoa tindikali hiyo.
Kwa
mujibu wa polisi, alidaiwa kumpanua msichana huyo mdomo na kujaribu
kumimina tindikali hiyo ndani ya mdomo wake. Kiasi kidogo kilimwagikia
usoni mwa binti huyo na kupata majeraha ya kuungua kwa asilimia 10-15.
Madaktari sasa wanajaribu kutathmini kiasi gani cha madhara ya ndani ya mwili aliyopata.
"Sakhpal
anaonekana kuwa alipanga hayo kabla kutokana na kuwa amebeba kabisa
tindikali hiyo," msaidizi wa kamishna wa polisi Mahesh Patil, alieleza.
Taarifa
zinasema kwamba baada ya baba wa msichana huyo kulalamika kwa polisi
kuhusu mvulana huyo, wawili hao waliripoti kwenye kituo cha polisi na
'kuandika kwamba hawatakutana tena na suala hilo limeshapatiwa
ufumbuzi," alisema Deepak Bagawe, inspekta wa ngazi ya juu wa polisi wa
Gorai.
Mmoja wa jamaa wa binti huyo alieleza: "Hapo awali
tulifungua madai kuhusu kijana huyo. Alizoea kumtesa binti huyo na
kumpiga hadharani. Alifikia hata kumtishia kumuua yeye na baba yake."
Hali ya binti huyo inaimarika lakini bado hawezi kutoa maelezo, kwa mujibu wa polisi walionukuliwa.
Ripoti
zimedokeza kwamba baba wa msichana huyo anafanya kazi kwenye
halmashauri ya mji huo wakati baba wa mvulana huyo ameajiriwa na kampuni
binafsi
No comments:
Post a Comment