DAWA YA MGANGA YA KUWAROGA WEZI YAWAGEUKIA WANAFAMILIA HUKO BUTIAMA.....WAPAGAWA NA KUGEUKA VICHAA..!!


http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/1913436/highRes/542162/-/maxw/600/-/8wc0as/-/mwathirika.jpg
Matiko Joseph mmoja wa waathirika waliokunywa dawa akiwa amelazwa hospitali. Picha na Antony Mayunga.
Mwalimu aliyetumia uchawi kuwaroga wezi, amejikuta akiwaroga shemeji zake waliopata uchizi
Butiama. Ilikuwa kama simulizi ya kwenye filamu, baada ya mganga wa kienyeji aliyeletwa toka Kenya kuja kuwaroga wezi walioiba nyumbani kwa Mwalimu mstaafu, Raphael Omwando (60), baada ya dawa yake kuwatia uchizi ndugu wa mke mkubwa wa aliyeibiwa.
Mwalimu Omwando ambaye ana wake wawili alivamiwa na wezi waliomwibia pikipiki na mali nyingine, ikiwemo kumjeruhi yeye (Omwando) na mkewe mkubwa. Mke mdogo aliyemuoa hivi karibuni anaishi kwenye nyumba nyingine na
hakuweza kuvamiwa na wezi hao, lakini mke mkubwa alipigwa hadi kulazimika kupewa matibabu hospitali.
Watu walio karibu na familia hiyo walisema kutokuelewana kati ya mke mkubwa na mdogo, kulimfanya mke mkubwa aliyejeruhiwa na majambazi kumtuhumu mke mdogo kwamba alishirikiana na majambazi hao.
Filamu hiyo ya familia ilianza kwa ndugu wa mume (Omwando) wanaoishi Kenya, kuleta sangoma kwa ajili ya kubaini wezi waliomwibia ndugu yao.
“Sijui nimefikaje hapa hospitali…maana kumbukumbu zinaishia pale nilipolazimishwa kunywa dawa na mganga wa kienyeji (Sangoma) anayedaiwa kutokea nchini Kenya …ili wezi wa pikipiki na vifaa vya mwalimu mstaafu virudishwe,” hiyo ni kauli ya mmoja kati ya watu wanne waliolazwa hospitali kwa madai ya kurukwa na akili.
Wagonjwa hao ni vijana wanne wa Kijiji cha Kirumi  Kata ya Bukanga, Tarafa ya Makongoro, Wilaya ya Butiama, mkoani Mara waliolazwa hospitali ya Mkoa wa Mara baada ya kunywa dawa hiyo na kupoteza fahamu huku wakionekana kama mazuzu (Mazombi).
Waathirika

Matiko Joseph (25) anasema yeye alilazimishwa kunywa dawa nyingi pamoja na makapi yake,” …Baada ya kumtajia mganga hivyo akasema ninyi kunyweni nyingi…dawa ilikuwa na ukakasi ilinikereketa sana. Baada ya kunywa niliondoka lakini baadaye hali ikabadilika sana,” anasema na kuongeza,

“Nilishtukia niko hospitali tayari ikiwa ni siku ya pili …Nikisimuliwa ilivyokuwa nazidi kushangaa…huyo mganga alilenga kutuua kabisa….maana wakati anatoa dawa alisema atakayepata madhara hatapona hata akipelekwa wapi mpaka vitu virudi ama fedha…akaondoka kwenda Kenya na hakuacha simu wala jina lake kujulikana,” anasema Joseph huku akipumua kwa harakaharaka.

Tura Joseph (30) anasema wengine walikunywa kidogo lakini wao wana ndugu walilazimishwa kunywa zaidi kwa kile kinachodaiwa kuwa walihisiwa kula njama za kumdhuru shemeji yao, na ndiyo walidhurika zaidi.

Anasema baada ya kunywa alihisi kitu kinamkaba shingoni na kuishiwa nguvu, akawa hoi na kuanza kuongea maneno yaliyowatia shaka, ndugu wakawabeba kwa bajaji hadi hospitali.

No comments:

Post a Comment