HUU NDIO MWILI WA MAREHEMU MANGWEA UKIWA MONCHWARI....R.I.P MANGWEA..!!

KIFO CHA NGWEA: LADY JAYDEE NAYE ASITISHA SHOW YAKE

Mwanamuziki nguli wa muziki wa kizazi kipya nchini, mwanadada Judith Wambura Maarufu kama Lady Jaydee ametangaza kuahirisha shughuli ya maadhimisho ya miaka 13 tangu aanze muziki iliyokuwa imapangwa kufanyika Ijumaa hii ya Mei 31, 2013 katika mgahawa wake wa Nyumbani Lounge kupisha msiba wa kifo cha msanii Albert Robert Mangweha aliyeripotiwa kufariki nchini Afrika Kusini jana.

Judith amesema hayo muda mfupi uliopita (saa 3:52 asubuhi) wakati akihojiwa katika kipindi cha Super Mix ya East Africa Radio na mtangazaji Zembwela.
  
Jaydee ameeeleza uamuzi wake wa kutitisha show hiyo kuwa unalenga kutoa nafasi kwa wafiwa wote na wadau wa tansnia ya muziki na wapenzi wa Mangwea kumaliza taratibu za kumsitiri kipenzi chao na kueleza kwamba tarehe nyingine ya shughuli hiyo itatangazwa baadae.
Tangu amekaribishwa studio, Judith Wambura alionekana kuwa na majonzi sana kiasi cha kushindwa kuongea mara kwa mara na kukatisha mazungumzo yake kutokana na kukabwa na kilio.

hawa ndio wa dau


ngwea.....

ngwea.......

ngwea....

ngwea...

ngwea........



Wakati Huo Huo Producer mkongwe katika game hii ya muziki, P-Funk Majani nae ameonesha ni jinsi gani alivyoguswa na na tukio hili la kuondokewa na msanii ambaye alikuwa ni rafiki yake wa karibu sana marehemu Albert Mangwair …

Majani ni producer pekee ambaye alishiriki kwa kiasi kikubwa kwa kuweza kufanya rapper Ngwair kutambulika katika game ya muziki wa Bongo Flava

Akiongea na mwandishi wetu kutoka GongaMx.Com, Majani ameeleza utayari wake katika kushirikiana na familia ya marehemu Albert Mangwair mpaka rafiki yake huyo atapozikwa

Mcheki MAJANI akiwa anaongelea suala zima kuhusina na msiba huu na utayari wake katika kushiriki

No comments:

Post a Comment