HIVI NDIVYO BABA MZAZI ALIVYOMCHOMA MWANAYE MWILI MZIMA AKIWA KWENYE HARAKATI ZA KUMTIBU FANGASI....!!

BABA mzazi  amejikuta akiingia matatani mara baada ya kumsababishia majeraha kadhaa mwanaye a kike wakati akijaribu kumtibu ugonjwa wa FANGASI ambao ulikuwa ukishambulia ngozi ya binti wake huyo kwa kiasi kikubwa cha mwili....

Akiongea na chanzo chetu cha karibu baba mzazi huyo ambaye hakutaka jina lake kutajwa alisema kuwa alifikia uamuzi huo mara baada ya kuona afya ya Ngozi ya mtoto wake huyo ikidorora siku hadi siku kutokana na maradhi hayo ya ngozi ambayo yalikuwa yamesababishwa na FANGASI ambao walikuwa wameiharibu Ngozi ya mtoto huyo kwa kiasi kikubwa.

"Nilichemsha maji ya moto na kumuamuru mwanangu angie humo kwani niliona kuwa ndio njia pekee ya kulitibu tatizo hilo kwasababu ametumia dawa nyingi za kienyeji lakini hazikumsaidia kabisa"... alisema baba mzazi huyo 


Baada ya kupata majeraha hayo mtoto huyo kwa sasa yupo chini ya Uangalizi wa madaktari Bingwa kwaajili ya matibabu zaidi, lakini mpaka sasa hakuna chombo chochote cha sheria kilichooneshania ya kumshtaki mzazi wa mtoto huyo kutokana na hilo ambalo amelifanya.




No comments:

Post a Comment