Hivi ndivyo Dr Steven Ulimboka anavyo onekana Sasa toka Wodini alipo lazwa

Ni imani yangu kwamba kupitia vyombo mbalimbali vya habari na mitandao jamii,unafuatilia tukio zima la kusikitisha la kutekwa nyara na kujeruhiwa vibaya kwa Dr.Steven Ulimboka hapo juzi. Kama bado hujasikia au kufuatilia kwa kina,Gazeti La Mwananchi linayo taarifa ndefu na pana ambayo unaweza kuisoma kwa kubonyeza hapa.
Lakini wakati mtaani kukiwa na kila aina ya tetesi na mazungumzo,kubwa zaidi ni kujua hali ya Dr.Ulimboka.Sote,bila shaka tunamtakia uponaji wa haraka. Hizi hapa ni picha kutoka alipolazwa(Muhimbili) ambazo zimetoka kwa Da Subi pale www.wavuti.com. Naelewa kwamba zinasikitisha na pengine zisingefaa kuwepo katika ukurasa wa mbele namna hii.Pamoja na hayo(na ninaomba radhi) zipo nyakati ambapo mambo mengine lazima yawekwe hadharani kama yalivyo.Zitazame na kisha tembelea www.wavuti.com uone video kidogo ikiwa na ujumbe kutoka kwa Dr.Ulimboka.